UONGOZI wa Muungano wa Wafanyabiashara wa Masoko Mkoa wa Dar es salaam MUMADA waliopo Soko la Kibasila wameilalamikia Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushindwa kurekibisha uchakavu wa miundombinu ya majitaka, mazingira pamoja na majengo ya soko hilo la Kibasila licha ya Manispaa hiyo kukusanya ushuru wa kutosha kuboresha hali ya mazingira katika soko hilo.
Akizungumza na Efm jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Muungano wa Wafanyabiashara Masoko kanda ya Ilala Issa Malisa amesema uongozi hauko tayari kuona kampuni binafsi zinapewa tenda ya kuchukua ushuru na kukusanya taka katika eneo hilo wakati Wafanyabiashara wa Soko hilo wanaweza kufanya kazi hiyo.