MANYARA: WADAU WA UKIMWI WAJIPANGA BAADA YA WAFADHILI KUTOTENGA FEDHA

MANYARA: WADAU WA UKIMWI WAJIPANGA BAADA YA WAFADHILI KUTOTENGA FEDHA

Like
349
0
Friday, 31 July 2015
Local News

WADAU wa ukimwi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wameazimia kujipanga kikamilifu kuhakikisha wanafanya jitihada za kupatikana kwa fedha za kuendesha bajeti ya ukimwi baada ya wafadhili kutotenga fedha.

 

Wakizungumza  leo kwenye mkutano wa wadau wa ukimwi wa wilaya hiyo uliofanyika katika mji mdogo wa Mererani, wamesema hadi sasa wafadhili waliokuwa wanawategemea hawajatenga fedha za kushughulika na ukimwi.

 

Mwenyekiti wa wadau hao Sihimu Hamis amesema sekta binafsi na serikali kwa kwa ujumla wanapaswa kujipanga ili kuhakikisha wanapata fedha za kuendesha shughuli za ukimwi na kuwasaidia watu wanaoishi na VVU na mitandao yao.

Comments are closed.