MAONI YA OMARY KATANGA KWA RAIS WA SIMBA EVANS AVEVA

MAONI YA OMARY KATANGA KWA RAIS WA SIMBA EVANS AVEVA

Like
471
0
Wednesday, 18 February 2015
Slider

Rais wa Simba Evans Aveva, huna budi kukumbuka hata kwa bahati mbaya badhi ya ahadi zako ulizozitoa wakati ukiomba ridhaa ya kuwa kiongozi wa juu wa Simba,ili mambo yaende sawa.

Ulitoa ahadi nyingi mno ikiwemo ya kuhakikisha unazoa pointi 3 katika kila mechi,utaleta maendeleao ndani ya klabu,utaifanya simba kuwa ni moja ya klabu inayoheshimika ndani na nje ya nchi,utaongeza idadi ya wanachama,pia utahakikisha unavunja makundi yote na kuwaunganisha wanachama kuwa simba moja.

Hebu tuliangalie hili la kuvunja makundi-wanachama wa simba uliowatimua uanachama kwa maelezo kwamba umetakiwa kufanya hivyo kwa matakwa ya katiba,ndani yao wapo waliowahi kuwa wanachama kabla yako,kitendo cha kuwaondoa ni sawa na kuchimbua na kuiangamiza mizizi ya muhimili wa klabu ya simba.

Hakuna ubishi kwamba simba iliundwa na kikundi cha watu wachache na baadaye wakaongezeka na wengine kiasi cha kufikia hatua ya kugawana madaraka na kutunga sheria na kanuni zitakazoiongoza klabu,na usipokumbuka hili hakika utakwama katika uongozi wako.

NAKUSHAURI-kaa na kamati yako ya utendaji,chukueni katiba iangalieni upya na mjaribu kushauriana ni jinsi gani ya kuwarejesha wanachama hao uliowafukuza,hakikisha kwamba jambo hili linafanyika ndani ya nyumba yenu (Simba) na msikubali kuingiliwa na mtu yeyote toka nje.

Kwa kufanya hivyo ni dhahiri kwamba mtakuwa na jambo moja tu la kujadili,nalo si jingine bali ni SOKA PEKEE.

Maoni haya yanapatikana pia kwenye ukurasa wake wa facebook ambao ni Mlindamlango

Comments are closed.