MAPAMBANO YA RISASI YATAWALA KASKAZINI MWA MJI WA PARIS

MAPAMBANO YA RISASI YATAWALA KASKAZINI MWA MJI WA PARIS

Like
233
0
Wednesday, 18 November 2015
Global News

LIMETOKEA tukio la ufyatulianaji mkali wa risasi kaskazini mwa Paris katika mtaa wa Saint Denis huku ripoti zikisema kuwa operesheni ya polisi kuhusiana na mashambulio ya Ijumaa inaendelea.

Shirika la habari la AFP limeeleza kuwa Abaaoud Abdelhamid, anayedaiwa kupanga mashambulio hayo, ndiye aliyekuwa akisakwa kwenye operesheni hiyo mtaa wa Saint Denis.

Video iliyoonyeshwa na vituo vya televisheni vya BFMTV na iTele zimeonyesha watu walioshuhudia tukio hilo wakisema kuwa milio ya risasi ilianza kusikika saa kumi unusu alfajiri kwa saa za Ufaransa.

Comments are closed.