MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAPELEKEA VIFO VYA NG’OMBE SABINI NA TISA MVOMERO

MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAPELEKEA VIFO VYA NG’OMBE SABINI NA TISA MVOMERO

Like
345
0
Wednesday, 30 December 2015
Local News

JUMLA ya ng’ombe sabini na tisa zimeuawa kwa kipindi kinacho ishia mwezi Desemba mwaka huu   kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji yaliyotokea kwenye kijiji cha Dihinda  Tarafa ya Turiani Wilaya ya Mvomero  Mkoani Morogoro.

Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasilano kutoka Wizara ya Mifugo ,Kilimo na Uvuvi ,JUDITH MHINA amesema kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa haki za wanyama hususani  ng’ombe katika wilaya hiyo kwani wanyama hao wamekuwa wakiuawa bila sababu maalum.

JUDITH ameeleza  kuwa kutokana na kuwepo kwa migogoro hiyo baina ya wakulima na wafugaji wizara imeamua kushirikisha wizara nyingine ikiwemo wizara ya ardhi ili kuweza kutenga na kuanisha matumizi bora ya ardhi ili kuweza kuepukana na migogoro hiyo.

Comments are closed.