RAIS wa China Xi Jinping anatarajiwa kukutana na Rais wa Taiwan, Ma Ying-Jeou siku ya Jumamosi.
Shirika la habari la China, Xinhua limesema kuwa mkutano huo utakaofanyika Singapore, utakuwa wa kwanza tangu viongozi wa nchi hizo mbili walipokutana mwaka 1949, baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Awali serikali ya Taiwan ilitangaza kuhusu mkutano huo, ikisema viongozi hao wawili watajadiliana kuhusu masuala muhimu ikiwemo kuimarisha amani kwenye eneo la Taiwan na kwamba utafungua njia mpya ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili.