MAREKANI: DONALD TRUMP ATANGAZA KUFUKUZA WASYRIA IWAPO ATAPATA RIDHAA YA KUWA RAIS

MAREKANI: DONALD TRUMP ATANGAZA KUFUKUZA WASYRIA IWAPO ATAPATA RIDHAA YA KUWA RAIS

Like
263
0
Thursday, 01 October 2015
Global News

DONALD TRUMP amesema atawafukuza wakimbizi kutoka Syria walioko nchini Marekani iwapo atakuwa rais.

Bilionea huyo, ambaye kwa sasa anaongoza kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Republican amesema katika mkutano wa kisiasa kuwa akishinda watarudi kwao.

Matamshi hayo ni tofauti na aliyoyatoa mapema mwezi huu akihojiwa na Fox News aliposema Marekani inafaa kuwapokea wakimbizi zaidi.

Comments are closed.