MAREKANI: KIJANA ALIYEUNDA SAA ADAI FIDIA

MAREKANI: KIJANA ALIYEUNDA SAA ADAI FIDIA

Like
284
0
Tuesday, 24 November 2015
Global News

MVULANA mwenye umri wa miaka 14 aliyejipatia umaarufu baada ya kukamatwa kwa kupeleka saa ya kujitengenezea shuleni, anadai fidia ya dola za marekani milioni 15.

Ahmed Mohammed alitiwa mbaroni na polisi wa mji wa Irving, jimbo la Texas nchini Marekani baada ya saa yake kudhaniwa kuwa kilipuzi na baadaye akafukuzwa shule.

Mawakili wake wanadai dola milioni 10 za marekani kutoka kwa mji wa Irving na dola milioni5 kutoka kwa shule ya Irving Independent, wakisema Ahmed alifedheheshwa na kuathirika kisaikolojia.

Comments are closed.