MAREKANI KUCHUNGUZA MAUAJI YA WANAFUNZI WATATU WA KIISLAMU

MAREKANI KUCHUNGUZA MAUAJI YA WANAFUNZI WATATU WA KIISLAMU

Like
192
0
Thursday, 12 February 2015
Global News

POLISI nchini Marekani inachunguza iwapo mauaji ya wanafunzi watatu wa Kiislamu siku ya Jumanne yalichochewa na chuki dhidi za kidini, wakati ambapo miito inazidi kutolewa kwa mauaji hayo kuchukuliwa kama kosa la chuki.

Mtu aliefanya mauaji hayo Craig Stephen Hicks mwenye umri wa miaka 46, ameshtakiwa kwa makosa matatu ya mauaji ya daraja la kwanza, baada ya mauaji hayo katika mji wa Chapel Hill, kusababisha ghadhabu miongoni mwa Waislamu duniani kote.

Polisi imesisitiza kuwa uchunguzi wa awali ulionyesha mgogoro kati ya Hicks na wahanga wake juu ya maeneo ya maegesho ndiyo ulichochea mauaji hayo, yaliyogharimu maisha ya Deah Shaddy Barakat mwenye umri wa miaka 23, mke wake Yusor Mohammad mwenye miaka 21, na shemeji yake Razan Mohammad Abu-Salha mwenye umri wa miaka 19.

Comments are closed.