Marekani itafungua ubalozi wake mpya mjini Jerusalem hatua ambayo imesifiwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa.
Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner.
Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria.
Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umewakasilisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye.
Ambao waliudhibiti toka mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya kati, na inahutaja mji huo kuwa wake na usiogawanywe
Hatua hiyo ya Trump ya mwaka uliopita ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ilivunja msimamo wa Marekani kwa suala la mji huo na kwenda kinyume na misimamo ya nchi zingine duniani.