MAREKANI KUIMARISHA MASHAMBULIZI YA ANGA DHIDI YA IS SYRIA NA IRAQ

MAREKANI KUIMARISHA MASHAMBULIZI YA ANGA DHIDI YA IS SYRIA NA IRAQ

Like
222
0
Wednesday, 28 October 2015
Global News

WAZIRI wa Ulinzi wa Marekani Ashton Carter amesema Marekani inapanga kuimarisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu nchini Iraq na Syria.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu masuala ya ulinzi, waziri Carter amewaambia maseneta kuwa majeshi ya Marekani yatailenga miundo mbinu ya mafuta inayomilikiwa na kundi hilo na pia kuimarisha mafunzo ya wanajeshi wa mataifa ya Kiarabu wanaopambana ardhini na wanamgambo wa IS.

Marekani na Urusi zina malengo yanayokinzana katika eneo hilo, ambapo Urusi inamuunga mkono Rais wa Syria Bashar al-Assad, huku Marekani ikimtaka aondoke madarakani ili kuepusha umwagaji damu.

Comments are closed.