MAREKANI: MICHAEL BROWN AKUMBUKWA

MAREKANI: MICHAEL BROWN AKUMBUKWA

Like
221
0
Monday, 10 August 2015
Global News

MAANDAMANO yamefanyika nchini Marekani kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa kijana mweusi, Michael Brown ambaye hakuwa na silaha. Kijana huyo aliuawa na polisi mzungu katika mji wa Ferguson jimboni Missouri Agosti mwaka uliopita.

Miezi michache iliyofuata, watu wengine kadhaa weusi wasio na silaha waliuawa na maafisa wa polisi katika miji mbali mbali ya Marekani, ikiwemo New York, Cleveland na Baltimore.

Mamia ya watu wamekusanyika katika mji wa Ferguson jana Jumapili, na kufanya matembezi ya kimya ambayo yaliongozwa na baba wa Michael Brown.

 

Comments are closed.