MAREKANI: MTU MWENYE SILAHA AFANYA SHAMBULIO KATIKA UKUMBI WA SINEMA

MAREKANI: MTU MWENYE SILAHA AFANYA SHAMBULIO KATIKA UKUMBI WA SINEMA

Like
258
0
Friday, 24 July 2015
Global News

POLISI katika jimbo la Louisiana nchini Marekani wamesema kuwa mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki amewafyatulia risasi raia katika ukumbi wa sinema na kumuua mtu mmoja na wengine sita wamejeruhiwa , na mshambuliaji mwenyewe pia amejiua. Walioshuhudia wanasema kuwa walimuona mtu mmoja, mzungu wa umri wa miaka 50 au zaidi, amejitokeza kunako dakika ishirini baada ya filamu kuanza , na kisha kuanza kufyatua risasi kiholela. Tukio hilo limetokea saa chache tu baada ya Rais Barack Obama kuzungumzia tatizo la udhibiti wa silaha nchini Marekani.

Comments are closed.