MAREKANI NA ISRAEL ZAKUBALIANA KUWEKA KANDO MVUTANO

MAREKANI NA ISRAEL ZAKUBALIANA KUWEKA KANDO MVUTANO

Like
234
0
Tuesday, 10 November 2015
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamekubaliana kuweka kando mvutano uliosababishwa na kutiwa saini makubaliano ya mradi wa nyuklia wa Iran na kuweka nguvu za pamoja kutetea maslahi ya nchi zao mbili katika eneo la mashariki ya kati.

 

Wakifanya mkutano wa pamoja kwa mara ya kwanza baada ya kupita miezi 13 katika Ikulu ya Marekani rais Obama amesema wazi kuwa

usalama wa Israel ndio suala muhimu.

 

Rais Obama na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamekubaliana katika suala la Israel kupatiwa msaada wa kijeshi wenye thamani ya mabilioni ya dala.

 

Comments are closed.