MAREKANI: REPUBLICAN YASHIKA UDHIBITI WA BARAZA LA SENETI

MAREKANI: REPUBLICAN YASHIKA UDHIBITI WA BARAZA LA SENETI

Like
279
0
Wednesday, 05 November 2014
Global News

MATOKEO ya  awali  ya  uchaguzi  mdogo  nchini  Marekani yanaonesha  kuwa  chama  cha  Republican  kimechukua udhibiti  wa  baraza  la  Seneti kwa  kupata  kiasi  ya  viti  51 katika  baraza  hilo  lenye  viti 100.

Pia  chama  hicho kinaelekea  kupata  ushindi  wa kishindo  katika  baraza  la wawakilishi kwa  miongo  kadhaa. Warepublican wamefaidika  na  wimbi  la  kutoridhika  kwa  wapiga  kura na  kutoa  pigo  kwa  rais Barack Obama  ambalo litapunguza  uwezo  wake  wa  kupitisha  ajenda  zake katika  bunge.

Hata  hivyo kiongozi  wa baraza la seneti Mitch  McConnell  ameonyesha  hali  ya  maridhiano akidokeza  kuhusu  mfumo wa  vyama  viwili  nchini  humo.

Comments are closed.