MAREKANI: WAGOMBEA WA REPUBLICAN WANADI SERA ZAO

MAREKANI: WAGOMBEA WA REPUBLICAN WANADI SERA ZAO

Like
192
0
Friday, 07 August 2015
Global News

WAGOMBE 10 wanaoongoza katika kura za maoni za kumtafuta atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi mkuu wa Marekani jana usiku wamenadi sera zao katika mdahalo ulioonyeshwa kwenye televisheni.

 

Miongoni mwa walioshiriki ni bilionea Donald Trump ambaye kwa sasa ndiye mwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda, pamoja na senator Rand Paul wa jimbo la Kentucky, seneta wa Florida Marco Rubio na seneta wa Texas Ted Cruz.

 

Mdahalo huo uliodumu kwa masaa mawili uliwapa nafasi wagombea kutoa maoni yao kuhusu sera mbali mbali kama vile uchumi wa nchi, siasa za mambo ya nje na usalama wa taifa.

Comments are closed.