MAREKANI YAANZA MAZUNGUMZO YA KUIWEKEA VIKWAZO SUDANI KUSINI

MAREKANI YAANZA MAZUNGUMZO YA KUIWEKEA VIKWAZO SUDANI KUSINI

Like
175
0
Wednesday, 19 August 2015
Global News

MAREKANI imeanza mazungumzo na mataifa mengine wanachama kwenye Umoja wa Mataifa, juu ya uwezekano wa kuiwekea vikwazo Sudan Kusini, endapo serikali itashindwa kusaini makubaliano ya amani na waasi, ndani ya wiki mbili zijazo.

Mshauri wa usalama wa Rais Barack Obama, Susan Rice, amesema Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kwa mara nyingine ameivuruga nafasi ya upatikanaji wa amani.

Juzi Jumatatu, rais huyo wa Sudan Kusini aliishangaza Marekani na mataifa mengine yanayosimamia mazungumzo ya amani ya nchi yake, kwa kukataa kusaini makubaliano ya amani na waasi, licha ya muda wa mwisho uliowekwa na jumuiya ya kimataifa kumalizika.

Comments are closed.