MASHAMBULIZI ya angani yanayoongozwa na Marekani yamefanikisha kuwaua viongozi kumi wa kundi la itikadi kali la Dola la Kiisilamu katika kipindi cha mwezi uliopita wakiwemo wanaodaiwa kuhusika na shambulizi la mjini Paris au mashambulizi mengine ambayo yalipangwa kufanyika barani ulaya .
Afisa mmoja wa jeshi la Marekani nchini Iraq Kanali Steve Warren amesema wanamgambo hao waliuawa wakati wa mashambulizi ya anga yaliyofanywa nchini Iraq na Syria.
Kwa mujibu wa Warren mmoja wa walioua katika mashambulizi hayo ni Charaffe al Mouadan mshirika wa kundi la dola la kiisilamu nchini Syria ambaye anahusishwa moja kwa moja kuwa na mahusiano ya kigaidi na Abdel Hamid Abaaoud anaedaiwa kuongoza mashambulizi ya mjini Paris.