MAREKANI YAFANYA MSAKO WA MAABARA ZA DAWA ZA KULEVYA

MAREKANI YAFANYA MSAKO WA MAABARA ZA DAWA ZA KULEVYA

Like
174
0
Thursday, 03 September 2015
Global News

MAAFISA wa kupambana na dawa za kulevya nchini Marekani wamewatia mbaroni zaidi ya Watu tisini wakati wa msako wa maabara zinazojihusisha na dawa za kusisimua misuli.

Zoezi hilo lililofanyika katika majimbo ishirini lililenga dawa za kusisimua misuli ambazo zinatengenezwa na kusafirishwa kutoka China.

Mamlaka inayodhibiti matumizi ya madawa nchini Marekani,imesema Operesheni hiyo inayoitwa Cyber Juice imeanza mwezi Aprili na kulenga maabara zinazofanya kazi kwa siri zinazojishughulisha na dawa zinazopatikana kwa njia ya mtandao kutoka nchini China.

 

Comments are closed.