MAREKANI YAFANYA SHAMBULIZI LA KWANZA DHIDI YA IS

MAREKANI YAFANYA SHAMBULIZI LA KWANZA DHIDI YA IS

Like
240
0
Thursday, 06 August 2015
Global News

MAREKANI  imefanya  shambulio  lake  la  kwanza  la mabomu  dhidi  ya  wanamgambo  wa  Dola  la  Kiislamu kutokea  Uturuki.

 

Afisa  wa  Uturuki  amesema  ndege  isiyokuwa  na  rubani iliruka  kutoka  kituo  cha  jeshi  la  anga  kusini  mwa  nchi hiyo, na  kushambulia  maeneo  karibu  na  Raqqa  nchini Syria.

 

Viongozi  wa  mataifa  ya  magharibi  wamekuwa  wakiitaka Uturuki  muda  mrefu  kuchukua  jukumu  kubwa  zaidi katika  mapambano  dhidi  ya  IS, lakini  serikali  ya  Uturuki ilikaa  kando  kwa  miezi  kadhaa.

Comments are closed.