WIZARA ya Sheria ya Marekani imesema imefanikiwa kuzisoma data zilizohifadhiwa kwenye Simu ya iPhone, mali ya mmoja wa walipuaji katika tukio la mauaji la San Bernardino na kutangaza kuacha mpango wake wa kisheria dhidi ya Kampuni ya Apple.
Wakili wa Marekani Eileen Decker amesema kuna mtu aliisaidia idara hiyo kuifungua Simu hiyo ya iPhone bila kuathiri data zilizohifadhiwa.
Simu hiyo ni mali ya Rizwan Farook ambaye pamoja na mke wake wanatuhumiwa kuwaua watu kumi na nne kusini mwa California Desemba mwaka jana.