MAREKANI YAIPONGEZA BURKINA FASO

MAREKANI YAIPONGEZA BURKINA FASO

Like
353
0
Wednesday, 19 November 2014
Global News

SERIKALI ya Marekani imewapongeza wananchi wa Burkina Faso na viongozi wao kwa kutia saini mkataba utakao ongoza serikali ya mpito kuelekea serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Aidha Marekani imesema inampongeza Michel Kafando kwa kuapishwa kuwa rais wa mpito wa Burkina Faso na kuendeleza kasi iliyoanza wiki mbili zilizopita na kuwachagua watu watakaosaidia kuendesha serikali ya mpito ambao wamejitolea kujenga serikali ya kiraia na kidemokrasia.

Hata hivyo imeyataka majeshi ya Burkina Faso kuendelea na jukumu lao la msingi la kulinda mipaka ya Burkina Faso na usalama wa raia wake.

 

Comments are closed.