MAREKANI YAISHUTUMU URUSI KWA KUMPA MAPOKEZI YA HESHIMA RAIS WA SYRIA

MAREKANI YAISHUTUMU URUSI KWA KUMPA MAPOKEZI YA HESHIMA RAIS WA SYRIA

Like
241
0
Thursday, 22 October 2015
Global News

MAREKANI imeshutumu Urusi kwa kumpa mapokezi ya heshima Rais wa Syria Bashar al-Assad mjini Moscow.

Afisa wa wizara ya masuala ya ndani ya Marekani amesema taifa hilo halijashangazwa na ziara hiyo, lakini wasiwasi mkubwa kwa Marekani ni Urusi kuendelea kumsaidia kivita Assad kitendo ambacho inaamini kuwa  litaipa nguvu zaidi serikali ya Assad na hivyo kuendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Ziara hiyo ya kiongozi wa Syria ilifanyika wiki tatu baada ya Urusi kuanza kushambulia kwa ndege ngome za wapiganaji wa Islamic State na makundi mengine yanayopinga utawala wa Assad.

Comments are closed.