MAOFISA wa ulinzi nchini marekani wamekiri kuwa maabara kadhaa nchini humo zilipokea kimakosa sampuli hai za vidudu hatari vya kimeta zaidi ya mara mbili ya matarajio ya awali.
Pentagon imesema vifaa hamsini na moja katika majimbo kumi na saba nchini Marekani, pamoja na maabara zilizopo nchini Canada, Australia na Korea kusini walitumiwa sampuli hizo kutoka maabara ya jeshi la marekani.
Hata hivyo imeelezwa kuwa usafirishaji wa vidudu hivyo ulianza miongo kadhaa iliiyopita na kuendelea mpaka wiki iliyopita lakini hadi sasa hakuna mtu aliyeathirika wakati zaidi ya watu ishirini waliokuwa wakibeba sampuli hizo wamekuwa wakitibiwa kwa tahadhari.