MAREKANI YAMSHAMBULIA JIHAD JOHN

MAREKANI YAMSHAMBULIA JIHAD JOHN

Like
190
0
Friday, 13 November 2015
Global News

WANAJESHI wa Marekani wametekeleza shambulio la Anga lililomlenga mwanamgambo wa Islamic State kutoka Uingereza ajulikanaye  kwa jina la Jihadi John.

 

John alilengwa kwenye shambulio hilo lililotekelezwa karibu na mji wa Raqqa, nchini Syria kufuatia msimamo wake mkali pamoja na kuonekana kwenye video akiwakata shingo mateka wa kutoka mataifa ya Magharibi.

Afisa wa habari wa Pentagon-Peter Cook amesema kuwa wanaamini matokeo ya operesheni ya leo usiku italeta manufaa makubwa kulingana na malengo yao.

 

 

Comments are closed.