MAREKANI imethibitisha kuwa itaendeleza mazungumzo na Uturuki kuhusu kutoa majeshi yake yanayopambana na kikosi cha kigaidi cha Islamic State huko magharibi mwa Syria.
Msemaji wa idara ya Usalama wa nchi hiyo John Kirby amesema jitihada, nguvu na umoja unapaswa kuwepo kwa kuangazia zaidi katika maeneo muhimu hususani ya mipakani.
Hata hivyo Askari wa Kurdish PKK wamesema kuwa shambulio la Uturuki liko juu ya Uturuki ambayo inasimamia mapambano yake dhidi ya PKK ingawa Majeshi ya Kurdish bado yanapambana na wanamgambo wa kikundi cha kigaidi cha kiislamu cha Islamic State huku wakiilaumu Syria kwa kuchukua nafasi zao.