MAREKANI YATHIBITISHA KUFANYA SHAMBULIO SOMALIA DHIDI YA AL-SHABAB

MAREKANI YATHIBITISHA KUFANYA SHAMBULIO SOMALIA DHIDI YA AL-SHABAB

Like
316
0
Wednesday, 04 February 2015
Global News

MAAFISA  wa  Marekani  wamesema  vikosi  vya  jeshi  la  Marekani vimefanya  shambulio nchini  Somalia  dhidi  ya  kiongozi mwandamizi  wa  kundi  la  al-Shabaab.

Shambulio  hilo  lililofanywa  Januari  31  kwa  kutumia  ndege  isiyo na  rubani  kusini  mwa  mji  mkuu  Mogadishu  lilimlenga  Yusef Dheeq , mkuu  wa  operesheni  za  nje  na mipango  ya  upelelezi  na usalama  wa  kundi  hilo.  Hata  hivyo  haijathibitishwa  iwapo ameuwawa  katika  operesheni  hiyo.

Shambulio  hilo ni kampeni  inayoendelea  dhidi  ya kundi  la  al-Shabaab, ambalo  uongozi  wake  una mafungamano  na kundi  la  al-Qaeda.

 

Comments are closed.