MAREKANI YATOA ONYO KWA SALVA KIIR

MAREKANI YATOA ONYO KWA SALVA KIIR

Like
201
0
Tuesday, 18 August 2015
Global News

MUDA mchache baada ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kukataa kusaini makubaliano ya amani na hasimu wake, Riek Machar, Marekani imemtaka kufanya hivyo ndani ya wiki mbili, au akabiliane na hatua kali.

Machar alisaini hapo jana makubaliano ambayo yanakusudiwa kukomesha miezi 20 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini Rais Kiir amesema atarejea mjini Addis Ababa, baada ya siku 15 za mashauriano.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani John Kirby, amewaambia waandishi wa habari kuwa nchi yake inasikitishwa na kitendo hicho na kwamba itashirikiana na jumuiya ya kimataifa dhidi ya wale wanaohujumu mchakato wa amani wa Sudan Kusini.

Comments are closed.