MAREKANI YAUNGA MKONO UUNDWAJI WA JESHI LA PAMOJA KUPAMBANA NA BOKO HARAM

MAREKANI YAUNGA MKONO UUNDWAJI WA JESHI LA PAMOJA KUPAMBANA NA BOKO HARAM

Like
237
0
Thursday, 12 March 2015
Global News

MAREKANI imeunga mkono uundwaji wa jeshi la pamoja lenye askari hadi 10,000 katika eneo la Afrika Magharibi kwa lengo la kukabiliana na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Kiislamu Boko Haram.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani Mataifa 54 ya Umoja wa Afrika yameidhinisha jeshi hilo na kuuomba Umoja wa Mataifa kuridhia utekelezeji wake kwa dharura baada ya mashambilizi ya kundi hilo katika maeneo ya kaskazini mwa Nigeria na mataifa jirani ya Chad, Niger, Cameroon  katika lengo lake la kutaka kuanzisha taifa la Kiislamu.

 

Comments are closed.