MAREKANI YAWEKA MIKAKATI YA KUDHIBITI SILAHA

MAREKANI YAWEKA MIKAKATI YA KUDHIBITI SILAHA

Like
177
0
Wednesday, 06 January 2016
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama ametangaza hatua kadhaa zinazonuwiwa kukabiliana na matumizi mabaya ya silaha nchini humo, zikiwemo upatikanaji wa lazima wa leseni kwa wauzaji silaha na kufanya ukaguzi wa historia za wateja.

 

Obama ametangaza hatua hizo katika ikulu ya White House akiwa amezungukwa na manusura wa mashambulizi ya silaha yanayouwa karibu Wamarekani 30,000 kila mwaka.

 

Hata hivyo Obama amekiri kuwa hatua hizo alizozipitisha mwenyewe bila kulishirikisha bunge la Congress, hazitomaliza kabisa tatizo la matumizi mabaya ya silaha, huku Chama cha wamiliki wa silaha cha Marekani NRA, kikikosoa vikali hatua hiyo.

 

Comments are closed.