MASABURI AWACHAMBUA WATU WANAOJIPITISHA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

MASABURI AWACHAMBUA WATU WANAOJIPITISHA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

Like
268
0
Monday, 20 April 2015
Local News

MWENYEKITI  wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania-ALAT na Meya wa jiji la Dar es salaam,Dokta DIDAS MASABURI,amewachambua watu mbalimbali wanaojipitisha kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,ikiwemo ya Urais.

Dokta MASABURI amewataka Watanzania hasa vijana kuwa macho na watu wanaojipitisha mtaani na kujiita wao wagombea,huku akifafanua hivi sasa kuna wagombea na wale wanaoupapatikia uongozi nchini.

Mwenyekiti huyo  ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Baraza la Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi-UVCCM,Kata ya Sandal,ambapo Jumuiya hiyo ilikuwa ikitathimini ushindi walioupata kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuikomboa Mitaa 12 ndani ya Kata hiyo.

Comments are closed.