MASAIBU YA DIEGO COSTA YAONGEZEKA

MASAIBU YA DIEGO COSTA YAONGEZEKA

Like
304
0
Saturday, 03 October 2015
Slider

Kocha wa Uhispania Vicente de Bosque amemuacha nje mshambuliaji wa timu hiyo Diego Costa kwa mechi mbili za kufuzu kwa michuano ya mabingwa Ulaya mwaka ujao. Costa anahudumia marufuku ya mechi moja kwa kupata kadi nyingi za njano na alikuwa hawezi kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Luxembourg mnamo tarehe 9 mwezi Octoba. Del Bosque:Tumeona tusimshirikishe kwa mechi ya pili dhidi ya Ukraine. ”Hachezi vibaya”,Del Bosque alisema kuhusu Costa,na kuongezea kwamba Uhispania itamshirikisha katika mechi za usoni iwapo kila kitu kitakwenda sawa. Costa pia anahudumia marafuku ya mechi tatu nchini Uingereza kwa kusababisha ghasia katika ushindi wa Chelsea dhidi ya Arsenal baada ya kuweka mikono yake katika uso wa mlinzi Laurent Koscielny. ”Sikupendelea kile nilichokiona”,Del Bosque alisema kuhusu kisa hicho.”Sipendelei kile Costa alichokifanya”.

Comments are closed.