MASCHERANO: MPIRA SIO VITA, SIASA ZIWEKWE KANDO

MASCHERANO: MPIRA SIO VITA, SIASA ZIWEKWE KANDO

Like
279
0
Thursday, 02 July 2015
Slider

Nyota wa Argentina Javier Mascherano amewaomba wadau na wapenzi wa mpira wa miguu kuwa na utulivu kuelekea fainali kati yao na wapinzani wao Chile.

Timu hizi mbili zitakutana siku ya jumamosi huko Santiago huku mwenyeji wa michuano hiyo Chile wakiwa na shauku ya kumaliza karibu karne ya kushindwa kutwaa taji kwenye michuano mikubwa huku wakishuhudiwa na mashabiki wa nyumbani.

Wakati huohuo pia Argentina wanateswa na hamu ya kushinda taji la kwanza katika kipindi cha miaka 22, wakitazama zaidi ubora wa kikosi walichonacho ambapo hawatamani kuona wanakosa tena taji hili kubwa kama walivyokuwa wakikosa katika misimu ya nyuma

Mataifa haya mawili yamekuwa na migogoro ya kidiplomasia lakini  Mascherano ameyataka mataifa yote kuweka tofauti zao pembeni na kuungana katika michezo kwani mpira sio vita hivyo watumie mchezo huo kuimalisha ushirikiano wao

Comments are closed.