MASHABIKI WA MESSI NA RONALDO WAUWANA

MASHABIKI WA MESSI NA RONALDO WAUWANA

Like
380
0
Monday, 07 March 2016
Slider

 

Polisi nchini India wamemfungulia mashtaka ya mauaji mtu mmoja aliyemdunga chupa rafiki yake huku chanzo cha ugomvi kikiwa ni mabishano kuhusu nani kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji bora duniani.
Michael Chukwuma, 21 ambae ni raia wa Nigeria alimdunga kisu mwezake vilevile mnigeria ambaye walikuwa wakibishana naye.
Tukio hilo limetokea katika kitongoji cha Nallasopara
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP limeeleza kuwa Michael Chukwuma ameshtakiwa kwa kuua katika mji wa Mumbai ambapo Chukwuma na wenzake walikuwa wamemtembelea marehemu kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

”Mmoja wao alikuwa ni shabiki sugu wa mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Messi huku marehemu akimshabikia mfungaji mabao wa Ureno na Real Madrid Ronaldo”.
”Na kwa sababu ambayo haijulikani Chukwuma alimdunga marehemu mwenye umri wa miaka 34 kwa kisu na kumuua papo hapo.
Walioshuhudia wanasema kuwa marehemu alimrushia mshukiwa glasi usoni na mshukiwa akamshinda nguvu na kumdunga na ile glasi iliyovunjika.

Comments are closed.