MATAIFA 34 YA KIISLAM KUUNGANA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UGAIDI

MATAIFA 34 YA KIISLAM KUUNGANA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UGAIDI

Like
194
0
Tuesday, 15 December 2015
Global News

SAUDI ARABIA imetangaza kuunda muungano mpya wa kijeshi wa nchi 34 za kiislamu kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ugaidi.

Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia limesema kazi ya muungano huo itaratibiwa katika kituo cha pamoja mjini Riyadh.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, waziri wa ulinzi wa Saudia, Mwanamfalme Mohammed bin Salman, amesema kuwa muungano huo utaratibu juhudi za mapigano dhidi ya makundi yenye itikadi kali katika mataifa ya Syria, Iraq, Libya, Misri na Afghanstan.

Comments are closed.