MATAIFA TAJIRI NA MASKINI YABISHANA JUU YA NJIA ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

MATAIFA TAJIRI NA MASKINI YABISHANA JUU YA NJIA ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

Like
365
0
Friday, 12 December 2014
Global News

MAZUNGUMZO ya Umoja wa Mataifa kuhusu ongezeko la joto duniani yanakamilika leo mjini Lima, Peru, huku mataifa tajiri na maskini ulimwenguni yakibishana kuhusu aina ya hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi wanazostahili kuwasilisha katika mkutano wa kilele utakaoandaliwa mjini Paris Ufaransa, mwaka ujao.

Katika ziara fupi aliyofanya kwenye mazungumzo hayo yanayoendelea kwa mjini Lima, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry amezitaka serikali kumaliza kulumbana kuhusu ni nani anayestahili kufanya nini katika juhudi za kupunguza uchafuzi wa mazingira unaotokana na gesi ya kaboni inayolaumiwa kwa kusababisha ongezeko la joto duniani.

Mataifa tajiri yanasisitiza kuwa ahadi zinazotolewa zinastahili kulenga katika juhudi za kudhibiti gesi chafu na zinapinga masharti ya kujumuisha ahadi za kuzifadhili na kuzisaidia nchi masikini kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Comments are closed.