MATEKA WASEMA WALIKULA PANYA SOMALIA

MATEKA WASEMA WALIKULA PANYA SOMALIA

Like
298
0
Monday, 24 October 2016
Slider

Kundi la mabaharia ambao waliachiliwa huru Jumamosi baada ya kuzuiliwa na maharamia kwa miaka mitano nchini Somalia walikula hata panya ili waishi, mmoja wao ameambia BBC.

Arnel Balbero, kutoka Ufilipino amesema walikuwa wanapewa maji kidogo sana na walijihisi kama “wafu waliokuwa wakitembea” kufikia wakati wa kuachiliwa huru kwao.

Mabaharia hao walitekwa wakiwa kwenye meli mwaka 2012 kwenye pwani ya Ushelisheli na wakapelekwa Somalia bara na kuzuiliwa mateka.

Waliachiliwa huru Jumamosi. Taarifa zinasema waliokuwa wanawazuilia mateka walilipwa kikombozi.

Mabaharia hao walitoka Uchina, Ufilipino, Cambodia, Indonesia, Vietnam na Taiwan.

Bw Balbero alikuwa mmoja wa mabaharia waliokuwa kwenye meli ya FV Naham 3 ilipotekwa.

Meli hiyo ilizama mwaka mmoja baadaye na wakapelekwa Somalia bara kuzuiliwa.

Bw Balbero aliambia BBC kwamba kwa miaka minne unusu ambayo walikuwa mateka, yeye na wenzake walikuwa kama “wafu waliokuwa wanatembea.”

Alipoulizwa maharamia waliwashughulikia vipi, alisema: “Walitupa maji kidogo tu. Tulikuwa panya. Ndio, tulipika panya na kuwala huko msituni.”

“Tulikuwa tunakula kila kitu, kila kitu. Ukihisi njaa, unakula.”

 

Comments are closed.