MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI YAANZA KUTOLEWA

MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI YAANZA KUTOLEWA

Like
214
0
Monday, 26 October 2015
Local News

KUFUATIA kukamilika kwa zoezi la upigaji kura katika maeneo mengi nchini baadhi ya vituo vimeendelea kuhesabu kura ingawa kuna ushindani mkubwa kwa wagombea wa vyama mbalimbali.

Mbali na hayo hali ya usalama imeonesha kuimarishwa kwa kiwango kikubwa hali inayowawezesha wananchi kuendelea na shughuli za kawaida huku wakisubiri matokeo.

Hata hivyo baadhi ya vituo vya kupigia kura vimeanza kutoa matokeo ya awali ya ngazi za Udiwani, Ubunge na Urais ingawa zimejitokeza changamoto mbalimbali wakati wa kupiga na kuhesabu kura.

Comments are closed.