MATOKEO YA UCHAGUZI ZANZIBAR YAFUTWA

MATOKEO YA UCHAGUZI ZANZIBAR YAFUTWA

Like
269
0
Wednesday, 28 October 2015
Local News

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salim Jecha Salim ametangaza kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi visiwani humo kwa kudai kuwa uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi.

Akizungumza kupitia Televisheni ya serikali ya Visiwani Zanzibar-ZBC-Jecha amesema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi.

Aidha amesema kuwa ukiukwaji huo umetokana na baadhi ya makamishna wa Tume hiyo, kutotekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa kikatiba.

Comments are closed.