MATUMIZI MABAYA YA ARDHI NI TISHIO KWA MAENEO YANAYOZUNGUKA HIFADHI ZA JAMII

MATUMIZI MABAYA YA ARDHI NI TISHIO KWA MAENEO YANAYOZUNGUKA HIFADHI ZA JAMII

Like
484
0
Friday, 03 July 2015
Local News

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi mabaya ya ardhi yasiyozingatia mpango bora yamekuwa tishio kwa maeneo yanayozunguka hifadhi za jamii.

Nyalandu ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano kati ya  Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori –WMAs– uliofanyika jijini Arusha ambapo amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu  utakaorithiwa na vizazi vijavyo  mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi kuzingatiwa.

Aidha amesema kuwa ujenzi wa miji katika maeneo ya hifadhi ikiwemo Hoteli na kumbi za starehe unaathiri shughuli za uhifadhi na kuwataka wadau wa utalii kugawanya uwekekezaji  kwa kuwekeza nje ya hifadhi.

DSC_0567 3

Comments are closed.