Maulid Kitenge Ajiunga Rasmi EFM

Maulid Kitenge Ajiunga Rasmi EFM

Like
739
0
Wednesday, 20 August 2014
Slider

Mtangazaji mahiri wa michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam.

Kutokana na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha redio one,ndie mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza kufurahishwa kwakwe kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.

“Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu na anatarajia kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo.

Maulidi Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji wa lio bobea katika fani hiyo akiwemo Dizo one,Dennis Sebo,Sos B,Kanky Mwaigomole na Dj Majay.

Comments are closed.