Watangazaji mahiri wa michezo nchini, Maulid Kitenge na Omari Katanga jana usiku wameanza kazi rasmi katika kituo chako cha Radio EFM.
Watangazaji hao mahiri ambao wote wamejiunga wiki hii watakuwa wakitangaza katika kipindi cha michezo cha E Sports kinachoruka hewani kuanzia mida ya saa moja kamili usiku. Kwa kuanzia pia Mtangazaji Maulid Kitenge alikuwa uwanja wa ndege wa Kimataifa jana usiku kukutangazia moja kwa moja yaani live kuwasili kwa nyota wa timu ya wakongwe wa real madrid.