MAUZO YA KAMPUNI YA APPLE YASHUKA

MAUZO YA KAMPUNI YA APPLE YASHUKA

Like
286
0
Wednesday, 26 October 2016
Slider

Kampuni ya Apple imeripoti kushuka kwa mapato yake ya mwaka kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2001. Matokeo ya robo ya mwisho ya mwaka wa fedha nchini Marekani imethibitisha mwenendo wa robo mbili zilizopita kuwa mapato yalishuka kwa asilimia tisa.

Mapato kutoka China ambako kuna soko kubwa yanaonyesha huenda yatashuka kwa asilimia kubwa. Faida nayo imeshuka kwa asilimia kumi na tisa kwa miezi mitatu ukilinganishwa na miezi hiyo hiyo kwa mwaka jana.

Wachambuzi wanasema kuwa ni dalili ya kuwepo kwa bidhaa nyingi za simu sokoni.

Robo ya mwisho inaisha muda mfupi baada ya kuongezeka kwa iphone 7, kunamaanisha kuwa matokeo ya mauzo katika bidhaa mpya hazitoshelezi katika takwimu za hivi karibuni.

 

Comments are closed.