MAWAKILI WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YA SHERIA

MAWAKILI WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YA SHERIA

Like
233
0
Wednesday, 16 December 2015
Local News

JAJI MKUU wa Tanzania Mheshimiwa Othman Chande amewataka Mawakili kote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya Sheria na kwamba wasisite kuwaeleza ukweli wateja wao wanaopeleka mashauri Mahakamani ili kuepuka kupoteza muda na gharama katika masuala yanayoweza kupatiwa ufumbuzi nje ya Mahakama.

 

Akizungumza na Mawakili wapya 104 waliohitimu Shule ya Sheria  kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, amesema kuwa msingi mkubwa wa kazi yao umejengwa katika uzingatiaji wa maadili ya taaluma ya sheria.

 

 

 

JAJ4

Mawakili wakiwa wamesimama mbele ya Jaji Mkuu kabla ya kuapishwa.

 

Comments are closed.