MAWAZIRI WA FEDHA WAWEKA MISIMAMO YAO JUU YA SERA ZINAZOWEKWA NA BENKI YA DUNIA

MAWAZIRI WA FEDHA WAWEKA MISIMAMO YAO JUU YA SERA ZINAZOWEKWA NA BENKI YA DUNIA

Like
218
0
Monday, 20 April 2015
Local News

WAKATI Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Kifedha la Kimataifa ikiendelea Mjini Washington DC,Mawaziri wa Fedha wameweka misimamo yao juu ya sera ambazo zinawekwa na Benki ya Dunia.

Akizungumza na Vyombo vya Habari,Waziri wa Fedha wa Tanzania SAADA SALUM MKUYA, amesema wao kama nchi wamewasilisha walichoona katika utekelezaji wa mipango ya Benki.

Amesema wanaishukuru sana Benki ya Dunia kwa kuendeleza mipango ya kuweza kusaidia nchi za Kiafrika ,hususan kwenye mipango ya kujenga Miundo Mbinu ya Kiuchumi kama vile Barabara, Kilimo pamoja na Miundo Mbinu ya Maji na umeme.

Comments are closed.