MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE URUSI NA UTURUKI WAKUTANA BELGRADE

MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE URUSI NA UTURUKI WAKUTANA BELGRADE

Like
187
0
Friday, 04 December 2015
Global News

MAWAZIRI wa mambo ya nje wa Uturuki na Urusi wamekutana mjini Belgrade, katika mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kati ya viongozi wa nchi hizo mbili tangu kudunguliwa kwa ndege ya Urusi na Uturuki wiki iliyopita.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alikutana na mwenzake wa Uturuki Mevlut Cavusoglu pembezoni mwa mkutano wa shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE.

Lavrov amesema alikutana na Cavusloglu baada ya kumuomba mara kadhaa kukutana naye lakini hakuna jipya lililotokana na mkutano wao.

Comments are closed.