MAWAZIRI WA ULINZI UJERUMANI NA IRAQ KUKUTANA

MAWAZIRI WA ULINZI UJERUMANI NA IRAQ KUKUTANA

Like
183
0
Tuesday, 27 October 2015
Global News

WAZIRI wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen anatarajiwa kukutana na waziri mwenzake wa Iraq kutafuta njia za kurekebisha hali inayosababisha watu kuikimbia nchi hiyo.

Akiwa mjini Baghad waziri huyo anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu Haider al Abadi na waziri wa ulinzi Khaled al Obeidi kwaajili ya mazungumzo hayo.

Akizungumza jana usiku kabla ya kuanza ziara yake hiyo von der Leyen amehimiza kuwepo kwa umoja ndani ya serikali ya Iraq na kuongeza kwamba maslahi ya Ujerumani katika eneo hilo hayatokani na watu kujitoa muhanga.

Comments are closed.