MAWAZIRI WASHIRIKI KUPANDA BANGI YA KIHISTORIA JAMAICA

MAWAZIRI WASHIRIKI KUPANDA BANGI YA KIHISTORIA JAMAICA

Like
491
0
Wednesday, 22 April 2015
Entertanment

Kwa mara ya kwanza katika historia huko Jamaica chuo kimoja cha utafiti wa mambo ya sayansi na tiba (UWI) University of the West Indies nchini humo kimepanda bangi katika ardhi ya chuo.

Siku ya tarehe 20 mwezi huu april kwenye kampasi moja ya chuo hicho bangi ilipandwa na waziri wa sayansi, teknolojia, nishati na madini mh. Phillip Paulwell lakini pia waziri wa sheria bwana Mark Golding pamoja na maofisa wa chuo hicho warishiki katika sherehe hizo zilizofanywa kwenye kitivo cha sayansi ya tiba na utafiti.

Huu unakuwa mmea wa kwanza wa bangi kupandwa kihalali katika ardhi ya nchi hiyo huku sherehe zake zikihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu pamoja na wadau mbalimbali.

Serikali ya Jamaica imekiagiza chuo hicho kuanza kufanya kilimo cha mmea huo kwa ajili ya tafiti za kitabibu lakini pia kuendeleza sekta ya bangi hiyo iliyohalalishwa kisheria kwa kasi kibiashara.

taarifa hii imetolewa

Jamaica Plants First Legal Ganja Plant

Comments are closed.