May aunga mkono uchunguzi dhidi ya Cambridge Analytica

May aunga mkono uchunguzi dhidi ya Cambridge Analytica

Like
378
0
Wednesday, 21 March 2018
Global News

Mkurugenzi mtendaji wa Cambridge Analytica, Alexander Nix,

Waziri wa Mkuu wa Uingereza Theresa May Jumatano ameunga mkono uchunguzi dhidi ya kampuni ya utafiti ya Cambridge Analytica, katikati ya mgogoro unaoikabili kwa madai ya kutumia vibaya takwimu za mtandao wa Facebook.
“Kile tulichokiona katika kampuni hiyo ya Cambridge Analytica, shutuma hizo ni wazi kabisa zinatia wasiwasi, ni sawa kabisa kwamba ni lazima uchunguzi kamili ufanyike,” May ameliambia Bunge la Uingereza.

Amesema kuwa hafahamu kama kulikuwa na mikataba yoyote kati ya serikali na kampuni ya Cambridge Analytica au makampuni yake tanzu.

Wiki hii madai kwamba kampuni ya utafiti ya Cambridge Analytica ilitumia taarifa za watu milioni 50 wanaotumia Facebook vibaya yamezua mjadala juu ya usimamizi wake katika mtandao huo wa kijamii.

Wachambuzi wa mambo ya mitandao wanasema takwimu ni hazina kubwa sana kwa mitandao ya jamii kwani husababisha biashara kufanya maamuzi ya kutumia mitandao hiyo kwa ajili ya matangazo ya kibiashara.

Comments are closed.