MAZUNGUMZO ya kusuluhisha mzozo wa Burundi yataanza tena leo mjini Kampala, chini ya usimamizi wa rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Rais Museveni aliteuliwa na Jumia ya Afrika Mashariki kuongoza mchakato wa amani ya Burundi, kufuatia machafuko yaliozushwa na uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kupigania muhula wa tatu, kinyume cha maana ya mapatano ya Arusha na katiba ya Burundi inayoruhusu mihula miwili.
Baada ya kuzinduliwa rasmi mjini Kampala leo, mazungumzo hayo yatahamishiwa Arusha Tanzania.